Klabu ya Tottenham hotspurs ya Uingereza imeanza mazungumzo na kocha wa zamani wa klabu ya Wolves Mreno Nuno Espirito Santo. Hatua hiyo imekuja baada ya klabu hiyo kushindwa katika majaribio kadhaa ya kuwanasa makocha wakubwa duniani ambao hawakuvutiwa na mipango ya klabu hiyo.
Nuno hakuwa kwenye orodha ya awali ya makocha wanaohitajika na Tottenham hadi alipowasili mkuruenzi mpya wa klabu hiyo Fabio Parattici ambaye ndiye aliempendekeza kuwa kocha mpya wa klabu hiyo ya kaskazini mwa London.
Nuno aliachana na klabu ya Wolves baada ya kumaliza kwa msimu wa ligi ya Uingereza 2020/2021 baada ya kuhudumu katika timu hiyo kwa miaka zaidi ya minne.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.