Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Princess, Aisha Masaka amefunguka kuwa, malengo yake makubwa ni kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi kama ilivyo kwa Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ aliyetimkia nchini Morocco.
Akizungumzia ishu hiyo Masaka alisema: “Mchezo wa soka umezidi kukua na kuwa biashara kubwa katika maeneo mbalimbali duniani, na kila ndoto ya mchezaji ni kuona anapata maslahi mazuri na kucheza soka la ushindani.
“Hivyo natamani nami nifikie kule ambako wamefika wenzangu ikiwemo Mwanahamisi”Alisema mshambuliaji huyo mkali kwa upande wa wanawake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.