Mabao ya Saimon Msuva 68′ na Abubakar Salum 90+4 yalitosha kuipa ushindi wa 2-1 timu ya taifa ya Tanzania(Taifa stars) dhidi ya Equatorial Guinnea katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya mataifa ya Afrika itakayofanyika nchini Cameroon 2021.
Stars ilitanguliwa kufungwa bao la mapema dakika ya 16 na Pedro Mba baada ya shuti kali kumshinda juma kaseja na kujaa wavuni.
Licha ya kucheza mpira wa kasi na pasi ndefu bado Stars haikufanikiwa kuliona lango la wapinzani hasa baada ya kufanikiwa kumdhibiti Mbwana Samatta huku Msuva na Farid Musa wakiwa hawapewi huduma stahiki.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mabadiliko ya mfumo ya kocha Ettiene Ndayiragije kutoka 4-4-2 kwenda 3-4-3 yaliipa ahueni Stars na kufanya watulie na mpira huku Kelvin Yondani akionyesha uhai baada ya kupangwa kama beki wa pembeni na kufanya Stars kuibuka na ushindi hivyo kuongoza kundi J baada ya kuwa na pointi 3.