Straika wa klabu ya Fc Lupopo ya nchini Congo Mpiana Mozizi anazihenyesha klabu za Simba na Yanga ambazo zinachuana vikali kumuwania staa huyo mkali wa nyavu.
Mozizi mwenye mabao 11 mpaka sasa katika ligi kuu nchini Kongo akiwa nyuma ya Jackson Muleka wa Tp mazembe mwenye mabao 12 anawaniwa na klabu hizo huku Simba sc wakiwa wa kwanza kuwasiliana nae huku Yanga nao wakipeleka jina kwa bosi wa Gsm ili kuanza harakati za usajili.
Hata hivyo klabu hizo inabidi zijipange kwani mchezaji huyo bado ana mkataba na klabu yake hivyo itahitajika dau kumng’oa.