Straika wa zamani wa klabu ya Yanga Kpah Sherman ameibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Malaysia baada ya kufunga mabao 14 katika mechi 19 akiichezea timu ya PKNS fc.
Sherman alihudumu Yanga 2014/2015 kwa takribani nusu msimu kabla ya kutimkia Mpumalanga Black Acces ya Afrika Kusini, akiwa Yanga SC alicheza mechi 27 na kuifungia mabao sita kwenye michuano yote.
Hata hivyo mabao ya staa huyo hayakutosha kuifanya timu hiyo imalize nafasi za juu baada ya kumaliza nafasi ya tisa kati ya timu 12.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.