Home SokaChan 2025 Taifa Stars Robo Fainali kwa Kishindo CHAN 2024

Taifa Stars Robo Fainali kwa Kishindo CHAN 2024

Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Madagascar

by Ibrahim Abdul
0 comments

Taifa Stars Robo Fainali kwa Kishindo

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa) imefanikiwa kunogesha kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Madagascar katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam siku ya jumamosi agusti 9 2025.

Katika mchezo huo kocha Hemed Morroco alifanya mabadiliko ya kumuanzisha beki Abdulrazack Hamza katika nafasi ya kiungo wa ulinzi akichukua nafasi ya Yussuph Kagoma aliyekua na kadi nyekundu huku anayemsaidia Ahmed Pipino akiwa na majeraha ambapo beki huyo wa Simba sc ana historia pia ya kucheza kama kiungo siku za nyuma.

Wachezaji wengine walianza katika nafasi zao kama ilivyokua katika michezo miwili iliyopita ambapo Stars ilipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Burkina Faso na 1-0 dhidi ya Mauritania michezo ambayo mastaa wa Stars walipambana kwelikweli kupata ushindi licha ya kukutana na ushindani mkali.

banner

Taifa Stars Robo Fainali kwa Kishindo CHAN 2024 - sportsleo.co.tz

MZIZE AIBUKA SHUJAA KIPINDI CHA KWANZA

Pamoja na kuwapo kwa sekeseke la usajili wake kwenda nje ya nchi mshambuliaji Clement Mzize alifanikiwa kufunga mabao mawili kipindi cha kwanza ambapo mabao hayo yalidumu mpaka dakika 90 za mchezo huo na kuwapa watanzania alama tatu muhimu na kufuzu robo fainali kwa kishindo ikiwa inaongoza kundi B.

Mzize alifunga bao la kwanza kwa kuunganisha mpira uliogonga mwamba baada ya Mudathir Yahaya Abbas kupokea pasi nzuri ya Idd Nado na kupiga shuti lililogonga mwamba na kurejea uwanjani ndipo Mzize alipouwahi na kufunga bao la kwanza kwa Taifa Stars dakika ya 13 ya mchezo.

Wakati Madagascar wakijiuliza walipokosea walifungwa bao la pili dakika ya 20 na Mzize safari hii akiunganisha kwa kichwa mpira wa faulo na kuwaacha mabeki wa Madagascar wakishangaa wasijue la kufanya na kuufanya uwanja wa Benjamini Mkapa ulipuke kwa furaha ambapo mashabiki wachache waliojitokeza walishangilia kwa nguvu zaidi.

Madagascar nao hawakua kinyonge kwani walipata bao la kwanza dakika ya 34 ya mchezo kupitia kwa Mika Gregasse na kuufanya sasa mchezo kuwa na umakini mkubwa ambapo kila timu ilicheza kwa tahadhari kubwa kuona namna ya kuchukua alama tatu japo Stars walifanikiwa kumaliza mchezo na ushindi.

Kipindi cha pili Stars ilikosa utulivu kwani ilifanikiwa kufika langoni mara kadhaa huku kitendo cha Feisal Salum kushuka chini kucheza namba sita na Hamza kutolewa nje kiliipa Stars balansi nzuri hasa katika umiliki wa mpira ambapo washambuliaji wake Mzize na Abdul Sopu walikosa utulivu tu wa kumalizia nafasi chache walizopata.

Taifa Stars Robo Fainali kwa Kishindo CHAN 2024 -sportsleo.co.tz

TAKWIMU ZA MCHEZO ZAZUNGUMZA ZAIDI

Stars ilifanikiwa kupiga mashuti 14 langoni mwa wapinzani wao ambapo walifunga mabao mawili pekee huku wageni wakipiga mashuti 12 na mawili yalilenga lango na moja kuzaa goli huku wakipiga pasi 423 dhidi ya 379 za Taifa Stars ambao wameonekana walicheza mpira wa moja kwa moja zaidi wakipiga pasi za kwenda mbele zaidi.

Timu zote zilikua na usahihi wa pasi kwa asilimia 77 huku kukiwa na kadi moja ya njano pekee katika mchezo huo na Madagascar wakicheza faulo mara 17 na Stars mara 15 na hakuna kadi nyekundu katika mchezo huo.

Stars sasa imebakisha mchezo mmoja dhidi ya Afrika ya kati huku ikiwa kileleni mwa kundi B na alama 9 dhidi ya wapinzani wake Mauritania mwenye alama nne Burkina Faso mwenye alama tatu huku Madagascar akiwa na alama moja na Afrika ya kati wakiwa hawana alama hata moja.

Taifa Stars Robo Fainali kwa Kishindo CHAN 2024 - sportsleo.co.tz

Taifa Stars Robo Fainali CHAN 2024 yajipangaje na mechi zijazo

Ushindi wa Taifa Stars kuelekea robo fainali CHAN 2024 haukuwa wa kusuasua kwani haikupoteza hata mechi moja. Maswali mengi yanaibuka kwa mashabiki kwamba je, gari limewaka kwa Stars na kuendelea kuwasha moto ikiwa ni mwiba kwa wapinzani anaokutana nao katika michuano hii, au tutegemee makubwa zaidi kutoka kwa kikosi bora kinacholiwakilisha taifa la Tanzania ambao ni wenyeji na waandaaji wa michuano hii ya CHAN 2024 ke-Tz-Ug (PAMOJA). Dua za watanzania wote wameelekeza kuiombea ushindi Taifa Stars kuelekea robo fainali na mechi zijazo za CHAN 2024. Tuendelee kujitokeza uwanjani kuipa nguvu timu yetu ya taifa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited