Tottenham Hotspur wanataka kumsajili winga hatari wa Wolverhampton Adama Traore katika dirisha dogo la uasjili mwezi Januari.(Fabrizio Romano)
Chelsea watatakiwa kumpa mkataba mnono mlinzi wa kati Antonio Rudiger ili kusaini mkataba mpya,vinginevyo ataondoka bure mwishoni mwa msimu huu.(Football Insider)
Real Madrid wana mpango wa kuwasajili kwa pamoja washambuliaji wawili hatari duniani Kylian Mbappe wa PSG na Erling Haaland wa Dortmund katika dirisha la usajili la majira ya joto.(ESPN)
Newcastle United wapo karibu kufikia makubaliano na mabingwa wa Hispania Atletico Madrid ili kumsajili mlinzi wa kulia Kieran Trippier.(The Athletic)
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tottenham wanataka kumsajili bure kiungo mshambuliaji wa FC Barcelona Philipe Coutinho lakini klabu yake wanataka paundi milioni 17 ili kumwachia.(El Nacional)
Manchester United wapo tayari kulipa ada ya paundi milioni 16 ili kununua mkataba wa mshambuliaji Julian Alvarez wa River Plate ya Argentina anayetajwa kuwa Tevez mpya huko kwao.