Home Soka Tetesi za soka leo Jumatano

Tetesi za soka leo Jumatano

by Sports Leo
0 comments

Real Sociedad wanaamini kuwa Manchester united itamruhusu kuondoka bure kiungo Juan Mata katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwakani.

Barcelona wanataka kuwasajili wachezaji wawili kutoka Chelsea Cesar Azpiliqueta na Andreas ambao mikataba yao inakaribia kuisha ndani ya viunga vya darajani.

Manchester united wanavutiwa na kutaka kumsajili mshambuliaji wa Bayern Leverkusen Florian Wirtz katika dirisha kubwa la majira ya joto barani Ulaya.

banner

Newcastle united wanafikiria kumsajili kiungo wa PSG Gergino Wilnadium miezi sita tu tangu aondoke kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kukosa namba ya kudumu huko Parc de Prince.

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel anataka kumsajili mlinzi wa kushoto wa Everton Lucas Digne baada ya Ben Chilwell kuthibitishwa atakuwa nje kwa muda mrefu zaidi baada ya kuumia goti.

Mshambuliaji a PSG Kylian Mbappe amesema kuwa hatojiunga na Real Madrid mwezi Januari kwani mawazo yake yapo kwenye kuwafungwa wafalme hao wa Ulaya kwenye hatua ya mtoano UEFA.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited