Home Soka Tetesi za soka Ulaya leo Jumatatu

Tetesi za soka Ulaya leo Jumatatu

by Dennis Msotwa
0 comments

PSG wanajiandaa kuwasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku kama mbadala wa Mfaransa Kylian Mbappe anayehusishwa kuondoka ndani ya miamba hiyo.Daily express)

Newcastle inataka kumsajili mshambuliaji wa Burnley Chris Wood pamoja na beki wa kati wa Monaco Benoit Badiashile mwenye thamani ya paundi milioni 35.(Daily telegraph)

Meneja wa Tottenham Antonio Conte ana mpango wakuwapiga bei nyota wawili kiungo Tanguy Ndombele na winga Steven Bergwin ili kupata fedha za kusajili wachezaji wapya ndani ya kikosi chake.(The athletic)

banner

Aston Villa wamepiga hatua kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa kushoto Lucvas Digne kutoka Everton ambaye anataka kwenda kucheza chini ya Steven Gerard.(skysports)

Manchester united haijapokea ofa yoyote ili kummuza kiungo wake Paul Pogba katika dirisha hili dogo la usajili,hata hivyo mchezaji huyo huenda akaondoka bure mwishoni mwa msimu mkataba wake utakapokuwa umekwisha.(Mail)

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited