Home Soka Tetesi za usajili Ulaya leo Jumanne

Tetesi za usajili Ulaya leo Jumanne

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Manchester united imefikia makubaliano ya kiasi cha paundi milioni 10 na Marseille kwaajili ya kumchukua kiungo mkabaji Boubacar Kamara.Huo utakuwa usajili wa kwanza kwa kocha mpya wa muda Ralf Rangnick ambaye anataka kuliimarisha eneo la kiungo wa chini ambalo limekuwa ni changamoto ya muda mrefu ndani ya klabu hiyo.

Kocha wa Arsenal anataka kuiimarisha kikosi chake Januari hii kwa kuwasajili wachezaji wawili kutoka Juventus.Wachezaji hao ni kiungo Arthur Melo ambaye amekosa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza pamoja na winga Msweden Dejan Kulusevki.

Barcelona wamefikia makubaliano binafsi na mshambuliaji wa Manchester city Ferran Torres ili kumsajili katika hili dirisha dogo mwezi Januari.Kinachosubiriwa ni kukubaliana ada ya uhamisho na klabu yake inayokadiriwa kufikia paundi milioni 50.

banner

Wakala wa beki wa kati wa Juventus Mathjis De Ligt Mino Raiola amesema kuwa mteja wake yupo tayari kuchukua hatua nyingine ya kisoka.Kinda huyo anahusishwa na kuhamia Barcelona ama Bayern Munich.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited