Home Soka Tetesi za usajili Ulaya leo Jumanne

Tetesi za usajili Ulaya leo Jumanne

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa Arsenal Maitland Niles yupo karibu kufikia makubaliano binafsi na AS Roma kwaajili ya kujiunga na klabu hiyo inayofundishwa na kocha Jose Mourinho katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.(mirror)

Mabingwa wa Ufaransa Lille wanahitaji kiasi cha Euro milioni 30 ili kumuuza beki wa Kiholanzi anayewindwa sana kwasasa barani Ulaya Sven Botmann(Tuttomercato).

Newcastle united wamemgeukia mlinzi wa kati wa FC Barcelona Samuel Umtiti anayepatikana kwa paunsi milioni 17 ili kumsajili katika dirisha dogo la usajili Januari(mirror).

banner

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amepitisha mpango wa timu hiyo kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Barcelona Phillipe Coutinho ili kumrejesha ligi kuu ya Uingereza.(Daily mail)

Real Madrid huenda ikahamishia nguvu zake kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic endapo dili la kusajili straika wa Borussia Dortmund likigonga mwamba(sky Italia).

Klabu ya Chelsea imeungana na Liverpool pamoja na Bayern Munich katika kuiwania saini ya winga wa Leeds united Ralphina,hata hivyo Bayern Munich wapo karibu zaidi kuinasa sana ya Mbrazil huyo.

Beki wa kushoto wa kimataifa wa Ufaransa na Everton Lucas Digne huenda akaondoka klabuni hapo mwezi Januari na kujiunga na Newcastle united baada ya Everton kumsajili mlinzi wa kushoto wa Ukraine Mykolenko.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited