Mgogoro unaoendelea kati ya mshambuliaji asiye na furaha wa Chelsea Romelu Lukaku huenda ukapelekea mchezaji huyo ajiunge na kocha wake wa zamani Antonio Conte katika klabu ya Tottenham.(Gazzetta Dela Sport)
Barcelona huenda ikafikiria kufanya mabadilishano ya kumpeleka Ousmane Dembele Man Utd na wao kumchukua Anthony Martial kama watashindwa kabisa kumuongezea mkatba mpya Dembele.(Ara-Catalan)
Newcastle United inataka kusajili wachezaji wasiopungua sita katika kipindi hiki cha dirisha dogo mwezi Januari,na wanaamini tayari watakuwa wamepata wawili akiwemo beki wa Atletico Madrid kabla ya tarehe 15 mwezi huu.(The Guardian)
Tottenham na West Ham nao wameingia katika vita ya kumsajili winga wa Wolves Adama Traore ambaye klabu yake inatarajia kupata paundi milioni 20 ili kuongeza fedha za kusajili wachezaji wengine.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Aston Villa ni moja kati ya vilabu vinavyohusishwa na kuwania saini ya kiungo wa Borussia Monchengladbach Denis Zakaria ambaye ni wa moto sana sokoni akihitajika pia Bayern Munich,Liverpool na Arsenal.(Mail)
Kocha wa Real madrid Carlo Ancelotti amesema kuwa huenda wakasubiri hadi mwezi Julai mwakani ili kumsajili mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe pindi mkataba wake utakapokwisha.(Marca)