Rais wa TFF Wallace Karia leo amefanya mazungumzo na Rais wa Chama cha Soka cha Umoja wa Nchi za Falme ya Kiarabu UAE Eng.Marwan Bin Ghalita mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Chama cha Soka UAE.
Katika mazungumzo hayo wamejadiliana kuhusu ushirikiano wa pamoja baina ya pande hizo mbili na wamekubaliana kushirikiana kwenye miradi mbalimbali.
Maeneo ambayo yataguswa ni Soka la Vijana, Mafunzo ya Makocha,Mafunzo ya Uongozi, Mechi za Kirafiki, mahusiano miongoni mwa timu za nchi hizi mbili na mafunzo ya waamuzi.
Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred na Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Umoja wa Nchi za falme za Kiarabu Mohamed Abdulla Hazzam Al Dhahari.