Home Soka TPLB Yamjibu Kocha Azam Fc

TPLB Yamjibu Kocha Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Bodi ya ligi kuu Tanzani imetolea ufafanuzi ombi la kocha mkuu wa klabu ya Azam fc Aristica Cioaba aliyeomba kuongezwa idadi ya wachezaji wa kufanyia mabadiliko kutoka watatu mpaka watano.

Kocha huyo alitoa ombi hilo ili kuepusha wachezaji kupata majeraha kutokana na kutocheza kwa muda muda mrefu baada ya ligi kuu kusimamishwa kupisha janga la ugonjwa wa corona huku wakitakiwa kucheza mechi mfululizo endapo ligi itarejea.

Akijibu kuhusu ombi hilo mtendaji mkuu wa bodi hiyo Almas Kasongo alisema ni ngumu kubadili kanuni hasa katikati ya msimu lakini watalichukua na kulifanyia kazi ikiwezekana.

banner

“Mimi nafikiri tulichukue ili wakati wa uboreshaji wa kanuni zetu tuliwasilishe lakini sioni kama kuna hiyo nafasi katikati ya msimu. Kwahiyo tutakapotangaza maboresho ya kanuni ni vizuri tukalichukua hilo“, amesema Kasongo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited