Home Soka Tumpe Muda-Mkwasa

Tumpe Muda-Mkwasa

by Sports Leo
0 comments

Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa amewataka mashabiki wa timu hiyo kumpa nafasi mshambuliaji Yikpe Gnamien kwani kuendelea kumshambulia wanazidi kumchanganya

Kwa siku za karibuni Yikpe amekuwa akicheza chini ya kiwango kila anapopewa nafasi jambo linalowakera mashabiki wa timu hiyo

Tayari presha ya mashabiki dhidi yake imeanza kushamiri jambo ambalo linaweza kumvuruga zaidi

Mkwasa amesema Yikpe amekuwa akifanya vizuri mazoezi na ndio maana wamekuwa wakimpa nafasi mara kwa mara lakini wanashangaa kwenye mechi hali inakuwa tofauti

“Mara nyingi najiuliza tatizo ni nini, kwani mazoezini anafanya vizuri na kuonekana bora, lakini akipangwa katika mechi, anashindwa kuonyesha kile alichokifanya katika mazoezi,” amesema Mkwasa

“Nafikiri anahitaji muda, lakini pia huenda presha ya mashabiki na maneno yanayozungumzwa dhidi yake yanamkatasha tamaa,,naamini akishazoea na kukubali changamoto, atakuwa mzuri sana”

Kuna wakati kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael alikiri mshambuliaji huyo kuwa na mapungufu lakini akaahidi kumuimarisha

Aidha, Eymael alisema wakati mwingine analazimika kumtumia kutokana na uhaba wa washambuliaji

“Molinga na Tariq wakiwa majeruhi hatuna namna tunapaswa kumtumia Yikpe. Ni mchezaji ambaye anajituma sana uwanjani, ana mapungufu machache nadhani yanarekebishika, tumpe nafasi”

Cc:Vicentpage

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited