Shirikisho la soka nchini Uganda (Fufa) limemteua Johnny Mckinstry raia wa Ireland kuwa kocha wa Timu ya taifa ya Uganda (The cranes) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Kocha huyo mwenye miaka 34 amechukua nafasi ya Mfaransa Sebastian Desabre aliyejiuzuru baada ya timu hiyo kutofanya vyema katika michuano ya Afcon 2019 iliyofanyika nchini Misri
Kocha huyo aliwahi kuzifundisha timu za taifa za Rwanda na Sierra leone alikua akiifundisha klabu ya Saif sporting ya nchini Bangladesh.
“Bila shaka kazi hii ni (kuifundisha uganda) moja ya kazi bora za kimataifa hapa Afrika kwa maana ya mwelekeo na levo ya ushindani”Alisema kocha huyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kocha huyo atasaidiwa na Abdullah Mubiru mpaka pale atakapotaja benchi lake la ufundi na atakua na kibarua cha kuhakikisha timu hiyo inafuzu fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2021 nchini Cameroon ambapo timu hiyo ipo kundi B pamoja na Burkina faso,Malawi na mmoja kati ya South Sudan na Sychelles.