Wakati msafara wa kikosi cha Simba sc ukielekea jijini Mwanza kuwavaa Polisi Tanzania,mchezaji Ibrahim Ajib hajasafiri na kikosi hicho kutokana na kusumbuliwa na maumivu hali iliyomfanya kutohudhuria mazoezi ya timu.
Kwa mujibu wa kocha wa kikosi hicho Didier Gomez mchezaji huyo hakuhudhuria mazoezi ya siku mbili katika uwanja wa Mo Simba Arena hali iliyomfanya amuache katika kikosi hicho huku akitarajia kuungana nae jumapili katika maandalizi ya michezo mingine.
“Ajibu kama atakuwa na maendeleo mazuri ya kiafya tunategemea kuwa nae katika kikosi Jumapili na ataungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi nyingine zinazofuata,” alisema Gomes.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.