Msemaji mkuu wa Serikali Mheshimiwa Gerson Msigwa amesema kuwa ujenzi wa uwanja wa kimataifa wa michezo uliopangwa kujengwa makao makuu ya nchi Dodoma uko palepale na hivi karibuni utaanza kujengwa.
Ujenzi wa uwanja huo uliasisiwa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli likiwa ni ombi lake kwa mfalme wa Morocco Mohammed wa sita alipokuwa nchini kwa ziara maalum mwaka 2016.
Ukimya wa muda mrefu juu ya jambo hilo na wasiwasi wa Watanzania ndio umemuibua msemaji wa serikali na kusema kuwa ”dhamira ya kujenga uwanja wa mpira jijini bado ipo,serikali inakamilisha michoro ambacho mchakato huu ukikamilika,zabuni itatangazwa na ujenzi utaanza”.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Msigwa pia alisema kuwa serikali imepeleka Tsh Bilioni 1.5 kwenye Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kuimarisha michezo,aidha serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye nyasi za bandia ili kuimarisha miundombinu ya michezo.