Home Soka Wabrazil Simba Lawamani

Wabrazil Simba Lawamani

by Sports Leo
0 comments

Kufuatia kipigo cha mabao 2-1 walichokutana nacho simba sc dhidi ya Kmc hapo jana katika uwanja wa Chamazi baadhi ya wadau wa soka wamehoji kuhusu viwango vya wachezaji kutokana Brazil wanaoichezea timu hiyo.

Wachezaji hao Tairone Da silver,Wilker na Gerson Fraga wamekua gumzo kufuatia kipigo cha jana cha mabao yaliyofungwa na Kenny Ally ikionekana kuwa uzembe wa beki wa kibrazili ndio ulisababisha mabao hayo hasa bao la pili lililofungwa kwa shuti kali.

Wachezaji hao bado hawajawa na msimu mzuri klabuni hapo wakipambana ili kuzoea mazingira hasa hali ya hewa na lugha huku majeraha yakiwa ni sababu ya kutoonesha uwezo kwa baadhi yao.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited