Home Soka Wanyama Amkimbia Pogba

Wanyama Amkimbia Pogba

by Dennis Msotwa
0 comments

Kiungo wa Tottenham Victor Wanyama yuko mbioni kujiunga na timu ya Club Bruge ya Ubelgiji baada ya timu hiyo kukubaliana dau la paundi milioni 9 ili staa huyo ajiunge na timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo (Jupiler Pro).

Staa huyo mzaliwa wa Kenya hana budi kuihama timu hiyo baada ya kukosa namba mbele ya viungo Harry Winks na Tanguy Ndombele aliyenunuliwa kwa dau la paundi milioni 52 huku majeruhi yakitajwa kuwa chanzo cha kukosa namba kikosini.

Wanyama alijiunga na Tottenham mwaka 2016 akitokea Southampton iliyomununua kutoka Celtic na baadae ikamuuza kwa dau la paundi milioni 11 kwa klabu hiyo yenye makao makuu jijini London.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited