Winga wa klabu ya Fc Lupopo Manu Labota Bola ameamua kujiunga na Singida Fountain Gate Fc na kuikacha ofa ya Yanga sc na tayari dili hilo limeshakamilika ukisubiriwa utambulisho tu klabuni hapo.
Awali Yanga sc ndio ilikua ya kwanza kuonyesha nia ya kumsajili winga huyo lakini ilianza kusuasua kukamilisha usajili huo ndipo mabosi wa Singida Fg walipoamua kumpandia ndege mpaka nchini Congo Drc na kukamilisha usajili huo haraka.
Mabosi wa Singida Fg pamoja na kukamilisha dili hilo iliwalazimu kufanya kazi ya ziada ili kuvunja mkataba wa staa huyo ambapo walifanikiwa baada ya kuzungumza na tajiri wa klabu hiyo Jacques Kyabula Katwe ambaye pia ni gavana wa jiji hilo ambapo zaidi ya Tsh 250 milioni zilitumika kukamilisha dili hilo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Singida Fg ipo katika maboresho makubwa ya kikosi chake msimu huu ambapo pamoja na kusajili usajili wa maana dirisha kubwa sasa inafanya maboresho machache katika dirisha dogo la usajili.