Home Soka Yanga Sc 5-1 Hausing Fc

Yanga Sc 5-1 Hausing Fc

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya timu changa ya Hausing Fc uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam ikiwa ni mchezo wa hatua ya 32 bora ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam Sports Confederations.

Yanga sc ikianza na kikosi mchanganyiko kikiwa na mastaa wengi ambao huwa hawaanza kikosi cha kwanza mara kwa mara golini akiwepo Aboutwalib Mshery akisaidiwa na walinzi Kibwana Shomari,Gift Fred,Zawadi Mauya na Farid Musa huku eneo la kiungo likiwa na mastaa Jonas Mkude na Salum Aboubakary pamoja na Shekhan Ibrahim,Mahalatse Makudubela huku eneo la ushambuliaji likiongozwa na Jonas Mkude.

Jonas Mkude alianza kuiandikia Yanga sc bao la kwanza dakika ya 20 kwa shuti kali huku dakika ya 25 Skudu alifunga bao la pili huku Clement Mzize akifunga mabao matatu dakika za 27,33 na 57 ambapo Hausing Fc walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 70 kupitia kwa Tonny Jailos.

banner

Yanga sc sasa imefanikiwa kufuzu hatua inayofuatia ambapo itasubiri mzunguko ukamilike ili kujua itakutana na nani katika hatua inayofuatia.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited