Yanga sc bado ya moto baada ya jana kuifunga klabu ya Mbuni Fc inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza yenye maskani yake jijini Arusha katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mchezo ambao Yanga sc ililenga kuwaongezea utimamu wa mechi mastaa wake wasiopata nafasi ya kuanza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza ambapo wachezaji kama Erick Johora,Paul Godfrey,Mukoko Tonombe,Chrispine Ngushi,Balama Mapiduzi na wengineo wakianza mchezo huo.
Yanga sc ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ambayo yalipatakana kwa penati ambazo zote zilifungwa kiufundi na kiungo Mukoko Tonombe aliyecheza kama mlinzi wa kati sambamba na Ibrahim Bacca aliyesajiliwa hivu karibuni kutoka KmKm ya Zanzibar baada ya kufanya vizuri katika michuano ya kombe la mapinduzi.
Pia kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka hapo uwanjani ni pale alipoingia winga Chico Ushindi ambaye alichukua nafasi ya Deus Kaseke dakika ya 64 na kusababisha shangwe kwa mashabiki huku wakikoshwa na kiwango cha staa katika kuwalaghai mabeki.
Yanga sc imesalia jijini Arusha ikiendelea na maandalizi ya mechi dhidi ya Polisi Tanzania itakayochezwa siku ya jumapili Januari 23 katika uwanja wa ushirika mjini Moshi.