Klabu ya Yanga sc imeendeleza wimbi la ushindi ikiifunga timu ya JKT Tanzania kwa mabao 5-0 na kufanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini kwa mara ya kwanza katika raundi ya pili ya ligi kuu ya Nbc.
Ikiwa ndiye mwenyeji wa mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam Yanga sc ikianza na washambuliaji wawili Kennedy Musonda na Hafiz Konkoni iliwabana wageni licha ya kukosa nafasi za wazi ambapo iliwapasa kusubiri hadi mwishoni mwa kipindi cha kwanza kuandika bao lililofungwa na Stephane Aziz Ki.
Kipindi cha pili licha ya mwalimu Malale Hamsini kuwaingia Danny Lyanga na Said Khamis Ndemla bado Yanga sc waliendelea kutawala mchezo na pasi ya Nickson Kibabage ikamkuta Musonda ambaye alifunga bao la pili dakika ya 54.
Dakika kumi baada Yao Kwasi alipiga mpira mrefu uliojaa wavuni moja kwa moja na kuiandikia Yanga sc bao la tatu huku Max Nzengeli akifunga mabao mawili dakika za 79 na 88 na kuhitimisha ule ushindi mnono wa mabao matano katika michezo mitatu mfululizo.
Yanga sc sasa wapo kileleni mwa ligi kuu nchini huku wakiweka rekodi ya kufungua mabao kumi katika michezo miwili ya ligi kuu nchini.