Site icon Sports Leo

Yanga Sc Yaipiga 5 Polisi Tanzania

Klabu ya Yanga sc imeendelea kusimamisha mnara wa mabao matano baada ya kuibamiza Polisi Tanzania kwa mabao 5-0 katika mchezo wa kombe la shirikisho la Azam Sports hatua ya 32 bora uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Ikianza mchezo bila mastaa wake Maxi Nzengeli,Djigui Diarra,Dickson Job,Ibrahim Hamad,Yao Kouassi,Pacome Zouzou ambao walikua jukwaani,Klabu hiyo ilianza kupata bao mapema dakika ya 13 kupitia kwa Joseph Guede kisha Farid Mussa dakika ya 33 akafunga bao la pili na dakika ya 45 Guede akafunga bao la tatu.

Clement Mzize ambaye aliingia kipindi cha pili alifunga bao la tatu dakika ya 82 kisha Shekhan Ibrahim akafunga bao la tano kwa penati dakika ya 87 baada ya Mzize kuangushwa katika eneo la 18.

Kwa ushindi huo Yanga sc sasa imefuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ambapo sasa inasubiri mzunguko ukamilike kisha ianze mbio za kuitafuta robo fainali.

Exit mobile version