Imeelezwa Klabu Ya Yanga Imeanza Mazungumzo Ya Kupata Saini Ya Golikipa Wa Kimataifa Wa Mali Diarra Djidgui kuja kuchukua nafasi ya Golikipa Mkenya Farouk Shikhalo.
Taarifa Zaidi Zinasema Golikipa Huyo Mwenye Umri Wa Miaka 26 Ameandaliwa Mkataba Wa Miaka Miwili Mezani Tayari Kuwatumikia Wananchi Msimu Ujao.
Golikipa Huyo Anayekipiga Katika Klabu Ya Stade Malien FC Ya Hukohuko Nchini Kwao (Mali) ni Moja Ya Wachezaji Waliokiongoza Kikosi Cha Nchi Hiyo Kilichoshiriki Kombe La Dunia Kwa Vijana Chini Ya Umri Wa Miaka 20 Mwaka 2015.