Klabu ya Yanga sc imemtambulisha mshambuliaji Joseph Guede kama usajili wake wa mwisho wa dirisha dogo la usajili msimu huu akiwa kama mchezaji huru baada ya mchezaji huyo kumalizana na klabu ya Tulazpur ya nchini Uturuki.
Mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast amejiunga na Yanga sc kwa mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Hafiz Nkokoni ambaye kocha Miguel Gamondi amesisitiza kuwa haingii katika mfumo wake wa uchezaji na kuhitaji aletewe mshambuliaji mwingine.
Katika kipindi chake cha soka mchezaji huyo amewahi kuhudumu klabu za As Far Rabat ya nchini Morroco,Emirate Club ya Uarabuni na Tulazpur ya nchini Uturuki ambayo aliachana nayo tangu mwezi Septemba mwaka jana.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc sasa itakua na washambuliaji watatu wa katika wakiwemo Kennedy Musonda na Clement Mzize ambao watakua na kazi ya kufunga mabao ili kushinda makombe jangwani.