Klabu ya Yanga sc na Namungo Fc zimeshindwa kutambiana katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa jumamosi ya leo.
Mchezo huo licha ya kutawaliwa na kosakosa za mara kwa mara ulimalizika kwa suluhu huku Yanga sc wakinyimwa bao la wazi baada ya Yacouba Sogne kumalizia kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Saido Ntibanzokiza huku ukigongwa na Tuisila Kisinda na kumkuta mfungaji ambapo mwamuzi alidai ameotea.
Yanga sasa imebaki nafasi ya pili ikiwa na alama 56 huku Simba sc wakiwa na alama 61 pamoja na michezo mitatu mkononi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.