Home Soka Yanga Wasalimu Amri

Yanga Wasalimu Amri

by Dennis Msotwa
0 comments

Uongozi wa Yanga umewarejesha kikosini nyota wake watatu, Cleofas Sospeter, Ali Ali na Raphael Daudi ambao walikuwa wametolewa kwa mkopo kwenda vilabu vya Singida United na Jkt Tanzania.

Cleofas na Lothi walipaswa kujiunga na kabu ya Singida United wakati Ali Ali alitakiwa akaitumikie JKT Tanzania,Hata hivyo nyota hao walipinga kutolewa kwa mkopo wakiomba wapewe nafasi ya kupigania namba kikosini huku Ali Ali akisisitiza kupelekwa Kmc kama ikishindikana.

Ali na Cleofas leo wameshiriki mazoezi maandalizi ya mchezo dhidi ya Lipuli Fc ambao utapigwa kesho kwenye uwanja wa Taifa huku Loth ikiwa hajaonekana.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited