Home Soka Yanga yamaliza mwaka kileleni NPL

Yanga yamaliza mwaka kileleni NPL

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya soka ya Yanga imefunga mwaka 2021 na kufungua mwaka 2022 vizuri baada ya kupata ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya wauza zabibu Dodoma Jiji.

Mchezo huo wa mzunguko 11 wa ligi kuu ya NBC umefanyika katika dimba la Mkapa Jijini Dar es salaam na kushuhudia mabingwa hao wa kihistoria nchini wakiwapa mashabiki wake zawadi ya mwaka mpya kwa ushindi.

Magoli ya Yanga yaliwekwa kimiani na mshambuliaji Fiston Mayele dakika ya 41 akimalizia pasi ya Yassin Mustapha,Jesus Moloko dakika ya 56 akimalizia pasi ya Bangala,Justin dakika ya 70 kwa kujifunga pamoja na Khalid Aucho dakika ya 81 .

banner

Katika mchezo huo mlinda mlango mpya aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Aboutwalib Mshery alianza katika kikosi hicho na kucheza viuri huku usajili mwingine Sure Boy akiingia kipindi cha pili na kuamsha shangwe kwa wananchi waliokuwa uwanjani hapo.

Ligi hiyo itaendelea tena wikiendi hii kwa mchezo mwingine mkubwa kati ya mabingwa watetezi Simba sc dhidi ya matajiri wa Jiji la Dar es salaam Azam fc katika dimba la Mkapa majira ya saa moja usiku Jumamosi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited