Home Soka Yanga Yanyimwa Kiporo

Yanga Yanyimwa Kiporo

by Sports Leo
0 comments

Bodi ya ligi kuu ya Tanzania bara (TPLB) imeigomea klabu ya Yanga sc ombi la kusogeza mbele mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting ulipangwa kufanyika Agosti 28 kufuatia ombi la klabu hiyo  kusogeza mbele mchezo huo kwa kuwa inakabiriwa na ratiba ngumu ya michuano ya kimataifa.

Awali Yanga ilituma ombi hilo baada ya kukosa ndege ya kuwawahisha nchini baada ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Township Rollers utakaofanyika Agosti 24 hivyo kulazimika kurejea Agosti 27 siku moja kabla ya mchezo.

Afisa mtendajiKauli wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alitoa majibu hayo wakati alipokuwa akijibu kuhusu maombi ya uongozi wa klabu ya Yanga kubadilishiwa ratiba ya mechi yao ya ufunguzi.

banner

“Yanga walituandikia barua kuomba tusogeze mbele mchezo wao, sisi tumewajibu kuwa hatutobadilisha ratiba ya mchezo wowote wa ligi, wao wanasema wanacheza Agosti 24 hvyo wana muda mfupi wa kujiandaa. Lakini sisi ratiba yetu tulishaitoa“, amesema Wambura.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited