Hiyo ikiwa ni siku chache tangu Mghana huyo kuondoka uwanjani wakati timu hiyo ikiendelea na mchezo wake wa Nusu Fainali ya Kombe la FA walipocheza na Simba na kulala kwa mabao 4-1, baada ya kutolewe katika dakika ya 66 na Ditram Nchimbi kuingia kuchukua nafasi yake.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata na kuthibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, kiungo huyo bado ni mali yao hadi Julai 15, 2022, baada ya kuongeza mkataba wake wa miaka miwili.
Mwakalebela alisema kuwa kiungo huyo kama anafanya matukio ya kiutovu wa nidhamu kwa makusudi akitegemea uongozi utasitisha mkataba wake na kuondoka kama mchezaji huru, basi imekula kwake.