Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga umetangaza rasmi kuachana na wachezaji wake Ditram nchimbi pamoja na Adeyun Swalehe waliojiunga na klabu ya Geita Gold baada ya kumalizika kwa mikataba yao ndani ya mitaa ya Twiga na Jangwani.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia ukurasa rasmi wa instagram wa klabu ilisomeka
Taarufa hiyo imeonyesha wazi kubwa huenda klabu hiyo ikaendelea kupitisha panga ndani ya kikosi chake pamoja na kusajili majembe mapya ili kujiimarisha zaidi katika harakati zao za kupigania ubingwa wa ligi kuu.
Mabingwa hao wa kihistoria nchini watashuka dimbani siku ya Jumapili usiku katika dimba la Benjamin Mkapa kwaajili wa mchwezo wao wa mzunguko wa kumi wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Biashara United ya Mara.