Timu ya soka ya Yanga sc imewasili usiku wa leo kutoka nchini Botswana ilipokua imeenda kukipiga na Township Rollers mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0.
Timu hiyo ambao ni mabingwa mara 27 wa ligi kuu Tanzania bara wametua nchini saa saba usiku na kulakiwa na mashabiki wa timu hiyo ambao walijitokeza kuwapokea baada ya kuwa wamefanikiwa kufuzu kwende raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambapo watakutana na Zesco united ya Zambia.
Baada ya kutua timu hiyo iliunganisha kambini katika hotel ya Nefaland iliyopo Manzese jijini Dar es salaam ili kujiandaa na mchezo dhidi ya Ruvu shooting utakaopigwa siku ya jumatano.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.