Baada ya kuwa zimemaliza ratiba ya michuano ya kimataifa timu za Yanga sc na Azam Fc sasa zimeeelekeza nguvu zao katika mechi za ligi kuu bara ambapo timu hizo zinakabiliwa na michezo miwili miwili ndani ya siku nne.
Ratiba ya timu hizo ambazo zimetolewa katika mashindano ya kimataifa inaonyesha kuwa Azam fc itawakaribisha Ndanda fc kesho tarehe 02 mwezi wa kumi katika uwanja wa Chamazi huku baada ya siku mbili yaani tarehe 5 itawakaribisha Namungo uwanjani hapo.
Na kwa upande wa Yanga ambao baada ya kupoteza dhidi ya Zesco na kukosa nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika japo wana nafasi ya kuingia hatua hiyo katika kombe la shirikisho watawakaribisha Polisi Tanzania iliyochini ya Seleman Matola tarehe 03 mwezi huu uwanja wa Uhuru.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Baada yaa siku mbili watawakaribisha Coastal Union katika uwanja huo huo ili kujitengenezea mazingira ya kurudi juu katika msimamo wa ligi ambapo wapo mwishoni baada ya kucheza mechi moja waliyopoteza dhidi ya Ruvu Shooting.