Aliyewahi kuwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye alitimuliwa kikosini hapo amezungumzia ishu ya kufutwa kazi kwa Kocha Luc Eymael na kusema Yanga watabaki hivohivo kwa miaka mitano ijayo.
Zahera amesema “wakati mnatenda mabaya au kuzulumu watu Mungu atawaadhibu kwa hayo hivyo hawawezi kuwa na furaha moyoni wakati wanabeba damu mikononi”.
Kocha huyo msaidizi wa timu ya Taifa ya Kongo aliwahi kuwa kipenzi cha wanayanga kiasi cha kusaidia kuhamasisha mashabiki wa timu hiyo kuichangia klabu hiyo katika michezo mbalimbali.