Timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imetoka sare na timu ya taifa ya Sudan katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya chalenji uliochezwa katika uwanja wa KCCA nchini Uganda siku ya jumapili.
Zanzibar walikua wa kwanza kupata bao mwanzoni mwa kipindi cha pili likifungwa na Hamis Makame dakika ya 56 bao ambalo lilidumu hadi dakika ya 89 ambapo Sudan walijipatia goli likifungwa na Osman Yahya na mchezo kumalizika kwa sare.
Iliwalazimu Zanzibar kumaliza mchezo wakiwa pungufu baada ya Ahmada Ibrahim Hamad kupata kadi nyekundu dakika ya 83 ya mchezo.