Home Soka Aucho Kuwasili Leo

Aucho Kuwasili Leo

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa kimataifa wa Uganda na klabu ya Yanga Khalid Aucho atawasili nchini hii leo akitokea Uganda ambako alikwenda kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes).

Aucho alikuwa Uganda kwenye majukumu ya timu ya taifa lakini hata hivyo hakufanikiwa kuitumikia timu taifa kufuatia majeraha madogo ambayo aliyapata akiwa huko yaliyolifanya benchi la ufundi la timu ya taifa kuamua kuacha kumchezesha ili kumpa muda wa kupumzika.

Mwalimu msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amethibitisha kuwa kiungo huyo atawasili leo na atajiunga kambini moja kwa moja ili kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc utakaofanyika siku ya Jumatano Aprili 6 katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited