Home Makala Mnahesabu Lakini

Mnahesabu Lakini

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kupunguza pengo la alama kati yake na vinara wa ligi kuu nchini klabu ya Yanga sc kwa alama tatu na kufikia alama nane sasa.

Awali kabla ya Simba sc kucheza na Kagera sugar ilikua inazidiwa alama kumi na moja na Yanga sc lakini baada ya Yanga sc kupata suluhu dhidi ya Coastal union huku Simba sc ikifanikiwa kumfunga Kagera Sugar na kupunguza pengo hilo la alama huku wote wakiwa na michezo 23 ya ligi kuu.

Mabao ya John Boko na Kibu Dennis yalitosha kuipa Simba sc alama tatu katika mchezo huo na kufikisha alama 49 dhidi ya 57 za Yanga sc ambao wataivaa Dodoma Jiji ugenini jumapili ijayo.

banner

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited