klabu ya Simba itamkosa Mlinda mlango Aishi Salum Manula ambaye alipata majeraha kwenye vidole vya mikono mwishoni mwa wiki iliyopita kabla ya mchezo dhidi ya Geita Gold baada ya kuangukiwa na kioo kilimkata kidole cha mkono.
Beno Kakolanya ambaye amekaa langoni kwenye michezo yote ya Simba kwenye michuano hii msimu huu ataendelea na jukumu hilo kwenye mchezo wa leo dhidi ya watani wao Yanga sc utakaoanza mapema hivi leo.
Aidha Simba ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano hii atawakosa baadhi ya wachezaji wengine kama vile Hassan Dilunga,Clatous Chama,Jonas Mkude kutokana na kutokua fiti hasa baada ya kuwa na majeraha.