Home Makala Kocha la Viwango Latua Azam Fc

Kocha la Viwango Latua Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imemtambulisha kocha Dennis Lavagne kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo akichukua nafasi ya AbdiHamid Moallin ambaye alipangiwa majukumu mengine baada ya kumrithi George Lwandamina kwa kipindi kifupi msimu uliopita na msimu huu ambapo aliiongoza Azam Fc katika michezo miwili pekee.

Kocha huyo raia wa Ufaransa ni moja ya makocha wenye wasifu mkubwa barani Afrika akiwa na leseni ya juu ya ukocha (Uefa Pro Licence) na tayari amewasili nchini jana usiku na kupokelewa na mabosi wa juu wa klabu hiyo akiwemo Abdulkarim Amin Poppat.

Wasifu wa kocha huyo unaonyesha kuwa amefundisha vilabu vikubwa barani Afrika ikiwemo timu ya Taifa ya Cameroon,Usm Alger,Js Kabylie za nchini Algeria huku pia akifundisha nchini Tunisia katika vilabu vya  Etoile Du Sahel,Smouha ya nchini Misri pamoja na Al Hilal ya Sudan na Coton Sports ya nchini Cameroon.

banner

Mabosi wa Azam Fc wameamua kufanya uwekezaji mkubwa msimu huu wakishusha mastaa kadhaa wa Afrika Magharibi wakina Kipre Junior na Tape Edinho vipaji ambavyo vilitarajiwa kwenda barani ulaya hivyo kuwasili kwa kocha huyo ni mwendelezo wa klabu hiyo kusuka kikosi kikali kwa ajili ya msimu huu wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited