Home Makala Yacouba Aaga Yanga sc,Atua Ihefu Fc

Yacouba Aaga Yanga sc,Atua Ihefu Fc

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji Yacouba Songne raia wa Burkina Faso sasa rasmi amechana na klabu ya Yanga sc baada ya klabu hiyo kukosa nafasi ya kumsajili kutokana na idadi ya wachezaji wa kigeni kujaa klabuni hapo na tayari amejiunga na klabu ya Ihefu Fc kwa mkopo wa miezi sita.

Yacouba kipenzi cha mashabiki wa Yanga sc alipata majeraha mwanzoni mwa msimu uliopita lakini klabu hiyo iliamua kumtibu huku akipata mazoezi ya kutosha ili kurejesha ubora wake katika kambi ya klabu hiyo iliyoko eneo la Avic Town Kigamboni kwa matarajio ya kurejeshwa kwenye timu pindi akiwa Fiti.

Licha ya kupona na kuonyesha kiwango kizuri katika michuano ya kombe la Mapinduzi staa huyo ameshindwa kusajiliwa na Yanga sc baada ya kuwa na changamoto ya idadi ya wachezaji wa kigeni kujaa kikosini ambapo kikanuni wanaruhusiwa wachezaji 12 pekee.

banner

Punde tu baada ya kumalizana na Yanga sc staa huyo alitua Ihefu Fc kwa mkataba mfupi wa miezi sita ili kujiweka fiti zaidi huku akisikilizia ofa mpya ama klabuni hapo au kwingineko.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited