Home Makala Phiri,Inonga Warejea Simba sc

Phiri,Inonga Warejea Simba sc

by Sports Leo
0 comments

Mastaa wa Simba sc Henock Inonga na Moses Phiri wamerejea uwanjani baada ya kuwa na majeraha yaliyiwaweka nje takribani wiki kadhaa na kuwafanya wakose baadhi ya michezo ya klabu hiyo hasa ile ya ligi kuu.

Wachezaji hao licha ya kurejea pia wameanza mazoezi kamili na kikosi hicho baada ya kumaliza siku kadhaa za mazoezi madogo madogo ambapo wameungana na Peter Banda ambaye amerejea tangu alipoumia katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars katika uwanja wa Liti.

Katika mazoezi ya leo asubuhi katika uwanja wa Mo Simba Arena Bunju wachezaji hao walishiriki kikamilifu hasa mazoezi ya mbio fupi fupi na ndefu na kurudisha tabasani kwa mashabiki wa klabu hiyo waliojitokeza mazoezini hapo hasa kutokana na umuhimu wa Phiri na Inonga.

banner

Bado haijafahamika kama watacheza mchezo ujao wa kombe la shirikisho dhidi ya Coastal Union wikiendi ijayo ama watahitaji muda kiasi ili kurejesha utimamu wa mwili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited