Home Makala Caf Waigomea Simba sc

Caf Waigomea Simba sc

by Dennis Msotwa
0 comments

Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) limeigomea klabu ya Simba sc kucheza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Raja Casablanca saa kumi jioni badala ya saa moja usiku.

Simba sc ilituma maombi hayo ili kuruhusiwa kucheza muda huo siku ya Jumamosi lakini Caf imetupilia mbali maombi hayo kwa kuwa kikanuni klabu hizo zinazoshiriki michuano hiyo ya ligi ya mabingwa ratiba kamili hupangwa na Caf na timu huwa watekelezaji tu.

Lengo kubwa la Simba sc ni kushinda mchezo huo ambapo kwa hali ya hewa ya jijini Dar es salaam kwa muda wa saa za jioni kunakua na joto kiasi ambacho wapinzani wao Raja Casablanca watapata shinda kuendana na kasi ya mchezo kutokana na hali ya hewa ya jua na joto tofauti na kwao ambapo kuna baridi la kutosha.

banner

Simba sc tayari imepoteza mchezo mmoja katika kundi C la michuano ya klabu bingwa ikikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Horoya Fc nchini Guinnea na wikiendi hii itatupa karata yake ya pili dhidi ya Raja Casablanca.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited