Wachezaji Fiston Mayele na Saido Ntibanzokiza wameingia katika vita mpya ya kuwania ufungaji bora wa ligi kuu ya soka ya Nbc baada ya kutofautiana kwa bao moja pekee huku ikiwa imesalia mchezo kwa kila timu ili kukamilisha ratiba ya msimu huu.
Awali Mayele alikua na mabao 16 huku Saido akiwa na 10 lakini katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania Saido alifanikiwa kufunga mabao matano na kufikisha mabao 15 na kuamsha upya vita ya mwishoni mwa msimu.
Kutokana na vita hiyo ya kuwania kiatu bora cha msimu imemlazimu Mayele kusafiri kuungana na timu jijini Mbeya ili kwenda kushiriki katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ili kujaribu kuongeza idadi hiyo ya magoli ili achukue tuzo hiyo ambayo aliikosa msimu uliopita dhidi ya George Mpole.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kwa upande wa Saido atakua na kibarua kigumu kuwafunga Coastal Union katika mchezo wa mwisho wa msimu utakofanyika jijini Dar es salaam.