Mshambuliaji wa klabu ya Al Hilal ya Sudan ambaye ni raia wa Congo DRC Makabi Lilepo rasmi ameomba kuondoka katika klabu hiyo ya nchini Sudan ili alinde kipaji chake baada ya nchi hiyo kukumbwa na vita hali iliyopelekea michezo kusimamishwa.
Pamoja na kuomba kuondoka,Tayari mchezaji anaviziwa na klabu za Yanga SC, Azam FC na Simba SC ambazo kwa wakati tofautitofauti zimewasiliana na uongozi wake kuulizia uwezekano wa kupata saini yake.
Tangu msimu uliopita Yanga Sc ilionesha nia ya kumsajili mchezaji huyo lakini ilizidiwa nguvu ya fedha na Al Hilal lakini sasa klabu hiyo ilikua tayari kuwaazima Yanga sc Mchezaji wao ila kwa makubaliano ya mkopo wa Miezi 6 kitu ambacho Uongozi wa Yanga Sc haukuridhia,
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.