Home Makala Bajeti Simba sc Yapaa

Bajeti Simba sc Yapaa

by Dennis Msotwa
0 comments

Awali mwezi Januari wakati wa mkutano mkuu wa klabu ya Simba sc uongozi wa klabu hiyo uliweka bajeti ya kiasi cha bilioni 13.7 kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa ambapo pia klabu hiyo itashiriki michuano ya Super League.

Bajeti hiyo mpya imepaa mpaka kufikia kiasi cha shilingi bilioni 24 ambapo imeongezeka kutokana na ushiriki wa michuano hiyo mipya ambapo jumla ya kiasi cha bilioni 5.8 kinatolewa na menejimenti  Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) ya michuano hiyo kwa ajili ya klabu kufanya maandalizi.

Akizungumza mbele ya mashabiki wa klabu hiyo waliopo bungeni ambao ni wabunge na waziri wakati wa chakula cha jioni cha mashabiki wa klabu hiyo,Afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Imani Kajula alisema kuwa klabu hiyo imekua ikitumia pesa nyingi katika kujiendesha ikiwemo gharama za kambi ambapo hutumia jumla ya milioni mia tano kwa ajili ya kambi pekee.

banner

“Bajeti ya klabu ya Simba sc msimu wa 2023/2024 ni Bilioni 23 na nadhani mlisikia bajeti wa wenzetu na sitaki kulinganisha mtgakumbuka wenyewe”

Simba sc imeanza mipango kabambe ya usajili kwa ajili ya msimu ujao ambapo sasa imeanza kupunguza baadhi ya wachezaji ambapo mastaa kama Jonas Mkude,Mohamed Outtara,Gadiel Michael,Victor Akpan,Erasto Nyoni,Beno Kakolanya,Nelson Okwa pamoja na baadhi ya watu wa benchi la ufundi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited