Ikiwa katika michezo ya kukiweka timamu kikosi hicho klabu ya Azam Fc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbuni Fc ya jijini Arusha katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini humo.
Mabao ya Azam Fc yalifungwa na Lusajo Mwaikenda kwa kichwa na Prince Dube huku wakifanikiwa kuonyesha kandanda safi mwanzo mpaka mwisho mwa mchezo huo uliokuwa wa kusisimua kwa pande zote mbili.
Azam Fc inajiandaa na ligi kuu nchini pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho la Azam Fc baada ya kutolewa katika michuano ya kimataifa ya kombe la shirikisho baada ya kutolewa na klabu ya Bahir Dar Kanema ya nchini Ethiopia.