Home Makala Afrika Mashariki Kuandaa Afcon 2027

Afrika Mashariki Kuandaa Afcon 2027

by Dennis Msotwa
0 comments

Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika Patrice Motsepe ametangaza kuwa nchi za Tanzania,Kenya na Uganda kwa pamoja zitaandaa fainali ya michuano ya kombe la mataiafa ya Afrika mwaka 2027 baada ya ombi lao kukubaliwa na sekretarieti ya shirikisho hilo.

Motsepe ametangaza hayo mbele ya wajumbe kutoka mashirikisho wanachama waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya shirikisho hilo nchini Misri ambapo sambamba na hilo pia aliitangaza nchini ya Morroco kuwa mwenyeji wa fainali hizo mwaka 2025 baada ya Guinnea kutokua tayari kwa miundombinu.

Michuano hiyo kwa mwakani inatarajiwa kufanyika nchini Ivory Coast kuanzia mwezi januari na februari huku Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizofuzu kushiriki michuano hiyo ikiwa ni mara ya tatu kushiriki michuano hiyo.

banner

Hii ni mara ya kwanza kwa nchi zote tatu za Afrika mashariki kupewa uenyeji wa michuano hiyo huku ikitarajiwa kufana kutokana na nchi ya Tanzania kuwa na mashabiki wengi wanaopenda soka.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kuwa wenyeji wa michuano mikubwa ya soka Afrika (AFCON2027), tukishirikiana na Kenya na Uganda. Nawapongeza nyote mlioshiriki kuhakikisha nchi yetu inapata fursa hii adhimu. Nawaagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha tunafanya maandalizi mazuri, ikiwemo kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, viwanja viwili vipya vya kisasa vya michezo Arusha na Dodoma”.Ulisomeka ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kupitia mitandao yake rasmi ya kijamii

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited