Home Soka Yanga sc Yajichimbia Kileleni

Yanga sc Yajichimbia Kileleni

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imejikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kuibamiza Mashujaa Fc kwa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Ikianza kikosi na washambuliaji wake wawili Joseph Guede na Clement Mzize Yanga sc ilishambulia kwa kasi sambamba na kumiliki mchezo hali iliyomlazimu kipa Erick Johora kufanya kazi ya ziada mara kwa mara ambapo dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza Maxi Nzengeli alifunga bao la kwanza kwa Yanga sc baada Johora kuutema mpira uliokua ukiingia wavuni.

Kipindi cha pili Yanga sc waliendelea kuwa bora mchezoni lakini mabadiliko ya Mwalimu Miguel Gamond ya kuwatoa Pacome Zouzou na Khalid Aucho yaliwapa unafuu Mashajaa ambao walikimilika kiungo na kusawazisha bao hilo kwa shuti kali la Emmanuel Mtumbuka dakika ya 65.

banner

Yanga sc walifanya mabadiliko ambapo Kennedy Musonda aliingia kuchukua nafasi ya Mzize ambapo aliongeza ubora na kasi ya ushambuliaji na kufanikiwa kupata bao dakika ya 85 likifungwa na Mudathir Yahya Abbas na kuihakikishia Yanga sc alama tatu muhimu.

Kutokana na ushindi sasa Yanga sc imefikisha alama 37 kileleni mwa ligi kuu nchini huku Mashujaa Fc ikiwa katika nafasi ya 15 ya msimamo ikiwa na alama 9 katika michezo 14 ya ligi kuu nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited